Menahemu
Mandhari

Menahemu (kwa Kiebrania מְנַחֵם, Mənaḥēm|Menaḥēm, yaani Mfariji) alikuwa mwana wa Gadi aliyepata kuwa mfalme wa Israeli kwa kumuua Shalumu (752 KK hivi). Ndipo alipoweza kutawala kwa ukatili miaka 10.
Biblia inamhukumu kwa kufuata sera ya kidini ya Yeroboamu I iliyowataka Waisraeli wamuabudu YHWH kwa sura ya fahali ya dhahabu katika mahekalu ya Dani na Beteli ili wasiende Yerusalemu, mji mkuu wa ufalme wa ukoo wa Daudi.
Habari zake zinapatikana hasa katika Kitabu cha Pili cha Wafalme 15:14-22.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]| Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Menahemu kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |