Nenda kwa yaliyomo

Richard Marx

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Richard Marx
Taarifa za awali
Jina la kuzaliwaRichard Noel Marx
Amezaliwa16 Septemba 1963 (1963-09-16) (umri 63)
Chicago, Illinois, Marekani
Kazi yakeMwimbaji, mtunzi wa nyimbo
AlaSauti, piano, gitaa
Miaka ya kazi1968–sasa
StudioCapitol, EMI, Manhattan, Signal 21, Zanzibar, Frontiers, Kobalt Label Services
WavutiKigezo:Official URL

Richard Noel Marx (alizaliwa 16 Septemba 1963) ni mwimbaji na mwandishi wa nyimbo kutoka nchini Marekani.[1] Ameuza zaidi ya albamu milioni 30 duniani kote.[2]

Mafanikio ya kwanza ya Marx kama mwandishi wa wimbo aliyeshika nafasi ya kwanza yalikuja mnamo 1984 kupitia wimbo wa "What About Me?", uliorekodiwa na Kenny Rogers, Kim Carnes, na James Ingram. Wimbo wake wa pili kuongoza chati ulikuwa "Crazy" wa mwaka 1985, ulioimbwa na Kenny Rogers. Albamu yake ya kwanza iliyoitwa kwa jina lake mwenyewe ilipata mafanikio makubwa mnamo 1987, na kibao chake cha kwanza, "Don't Mean Nothing", kilishika nafasi ya tatu kwenye chati za Billboard Hot 100.[3] Kati ya mwaka 1987 na 1994, alikuwa na nyimbo 14 zilizoingia kwenye 20 Bora, zikiwemo nyimbo tatu zilizoshika nafasi ya kwanza.

Marx ni msanii pekee wa kiume katika historia aliyefikisha nyimbo zake saba za kwanza kwenye 5 Bora za chati za Billboard. Ameshinda au kuandika jumla ya nyimbo 14 zilizoshika nafasi ya kwanza, kama mwimbaji, mwandishi au mtayarishaji. Kama mwimbaji, nyimbo zake zilizoshika namba moja ni pamoja na "Hazard", "Right Here Waiting", "Hold On to the Nights", "Endless Summer Nights", na "Satisfied".

Pia ameandika na kushirikiana kwenye nyimbo za wasanii wengine, ukiwemo wimbo wa "This I Promise You" wa NSYNC na "Dance with My Father" wa Luther Vandross. Marx amewahi kuteuliwa kuwania Tuzo za Grammy mara tano, na kufanikiwa kushinda Tuzo ya Grammy ya Wimbo Bora wa Mwaka kupitia wimbo wa "Dance with My Father".[4]

Diskografia

[hariri | hariri chanzo]

Albamu za Studio

[hariri | hariri chanzo]
  • Richard Marx (1987)
  • Repeat Offender (1989)
  • Rush Street (1991)
  • Paid Vacation (1994)
  • Flesh and Bone (1997)
  • Days in Avalon (2000)
  • My Own Best Enemy (2004)
  • Emotional Remains (2008)
  • Sundown (2008)
  • Christmas Spirit (2012)
  • Beautiful Goodbye (2014)
  • Limitless (2020)
  • Songwriter (2022)
  • After Hours (2026)
  1. ↑ "Biography & Career Highlights". Richard Marx Online. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-05-26. Iliwekwa mnamo 2026-08-02.
  2. ↑ "Live from The GRAMMY Museum: Richard Marx – GRAMMY Museum". Iliwekwa mnamo Septemba 19, 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. ↑ Feely, Paul (Machi 21, 2019). "Richard Marx 'Right Here Waiting' for another show in NH". UnionLeader.com.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. ↑ "Grammy Award results for Richard Marx". Grammy.com. Novemba 23, 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)