George Alencherry
Mandhari

George Alencherry (alizaliwa 19 Aprili 1945) ni Askofu mkuu kabisa Mstaafu wa Kanisa Katoliki la Kisiria la Malabar, baada ya kuhudumu katika nafasi hiyo kutoka 2011 hadi 2023. Pia ni kardinali wa Kanisa Katoliki.[1]
Alencherry alichaguliwa na Sinodi Takatifu ya Kanisa la Kisiria la Malabar mnamo 2011 kumrithi Varkey Vithayathil (aliyekuwa madarakani kutoka 1999 hadi 2011). Aliteuliwa kuwa kardinali na Papa Benedikto XVI tarehe 18 Februari 2012. Kabla ya kuwa Askofu Mkuu Kabisa, alikuwa askofu wa kwanza wa Thuckalay kuanzia 1997 hadi 2011.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Giraudo, Cesare (mhr.). "The Anaphoral Genesis of the Institution Narrative in Light of the Anaphora of Addai and Mari". Hugoye Journal of Syriac Studies. Edizioni Orientalia Christiana. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 29 Desemba 2021. Iliwekwa mnamo 29 Desemba 2021.
{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
| Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |