Nenda kwa yaliyomo

Adil Rami

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Adil Rami

Amezaliwa Adil Rami
27 Desemba 1985 (1985-12-27) (umri 40)
Bastia, Ufaransa
Nchi Ufaransa
Urefu 1.90 m

Adil Rami (alizaliwa 27 Desemba 1985) ni mchezaji wa zamani wa mpira wa miguu wa kulipwa kutoka nchini Ufaransa aliyecheza nafasi ya beki wa kati.

Rami alianza taaluma yake ya mpira wa miguu akichezea klabu ya Étoile Fréjus Saint-Raphaël bila malipo, iliyojulikana wakati huo kama ES Fréjus. Kwa sababu ya kucheza mchezo huo kama kitu anachokipenda pekee, alikaa misimu mitatu klabuni hapo akicheza katika ligi ya mpira wa miguu isiyo ya kulipwa ya Ufaransa ambalo ni daraja la nne la mpira wa miguu nchini Ufaransa. Mnamo mwaka 2006, Rami alipanda madaraja matatu baada ya kusaini mkataba na klabu ya Ligue 1 ya Lille. Akiwa Lille, Rami alikuwa mchezaji wa kikosi cha kwanza, akicheza mechi yake ya kwanza ya kulipwa mnamo Mei 2007. Alipewa jina la utani la "Shrek" na wachezaji wenzake pamoja na mashabiki wa Lille. Mnamo Januari 2011, Rami alijiunga na klabu ya Valencia ya Uhispania kwa mkataba wa miaka mine. Hata hivyo, alipelekwa mara moja kwa mkopo katika klabu yake ya zamani na alikuwa sehemu ya kikosi cha Lille kilichotwaa ubingwa wa ligi na kombe kwa msimu mmoja.[1]

Baada ya maombi ya awali kutoka Morocco kabla ya kuchaguliwa kwake kwa mara ya kwanza, Rami alichagua kucheza katika timu ya taifa ya Ufaransa. Alikuwa katika orodha ya awali ya kuchezea Ufaransa katika fainali za Kombe la Dunia la FIFA la mwaka 2010 lakini hakuingia katika kikosi cha mwisho. Rami alicheza mechi yake ya kwanza katika ngazi ya wakubwa mnamo 11 Agosti 2010 katika mechi ya kirafiki dhidi ya Norway.[2]

  1. ↑ "Adil Rami - National Football Teams". National Football Teams. Iliwekwa mnamo 19 Septemba 2026.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. ↑ "Adil Rami - FFF". FFF. Iliwekwa mnamo 19 Septemba 2026.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link) [dead link]
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Adil Rami kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.